KARIBU MKURANGA

Thursday, June 28, 2012

MKURANGA KUTEMBELEWA NA TUME YA MAREKEBISHO YA KATIBA, WADAU TUJITOKEZE.

Tume ya Marekebisho ya katiba nchini iliyo chini ya M/kiti wa Jaji mstaafu na waziri mkuu  mstaafu wa Tanzania Joseph Warioba watakuwa wilayani Mkuranga kwa siku 4 na vituo 8 tofauti kwa saa na tarehe zifuatazo:-

1. Mkuranga mjini 10/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
2. Vikindu tarehe 10/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
3. Kisiju tarehe 11/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
4. Magawa 11/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
5. Panzuo tarehe 12/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
6. Kimanzichana 12/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
7. Shungubweni 13/07/2012  kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
8. Nyamato 13/07/2012  kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni

Shime shime wana Mkuranga hususani wenye mwamko mkubwa tujitokeze tukaseme na kutoa maoni yetu katika katiba mpya, tuseme tunadhani nini sahihi, nini kiwepo na nini kisiwepo.

Mkuranga itajengwa na wana mkuranga, tuwakilishe vyema wilaya yetu, wajumbe wakitoka kwetu wakiri kuwa kweli walikutana na watu makini na sio vilaza, wapate taswira halisi ya watu wa Mkuranga hususani kizazi chetu chenye mwamko na hamasa kubwa.

Wasalaam,
M/Kiti wenu

No comments:

Post a Comment