KARIBU MKURANGA

Thursday, March 1, 2012

PROGRAMU YA KUFUNDISHA KWA KUJITOLEA KUZINDULIWA KESHO MKURANGA

Wana wa Kwetu ni faraja kubwa kwangu kuwatangazia kuwa kesho tarehe 04/03/2012 tutazindua Kampeni ya Kufundisha kwa kujtolea kwa wanafunzi wote wa shule za Sekondari za Wilaya ya Mkuranga. Kituo cha kwanza ambacho kitakuwa cha tathimini  (Pilot) kitakuwa Mwinyi Sekondari na baadae tutaanzisha vituo katika centers zingine kwa mgawanyiko wa Tarafa na hata Kata.

Programu hii itasimamiwa na kuendeshwa na Vijana wasomi wa wilaya ya Mkuranga kwa malengo makuu

  1. Kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo ya Kitaifa ya Kidato cha Pili na Nne
  2. Kujenga Hamasa kwa wanafunzi wa wilaya ya Mkuranga Kupenda kusoma na Kufaulu
  3. Vijana wasomi wa Mkuranga ikiwa ni sehemu yao ya ushiriki wa Maendeleo ya Nyumbani Kwao
  4. Vijana wasomi wazawa wa Mkuranga ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa rasilimali za Mkuranga zilizo wasomesha 
Wadau wote wa Maendeleo na Elimu wa Wilaya ya Mkuranga mnakaribishwa sana kuhudhuria na kutoa mawazo/michango ya namna ya kuboresha programu hii mpya wilayani kwetu

Tunatanguliza shukrani kwako wewe mdau wa wilaya yetu nasi tunaona fahari kubwa Mkuranga kuwa Kwetu

KIKAO KATI YA BODI YA SHULE YA MWINYI SEKONDARI, MENEJIMENTI NA WA WAKILISHI WA MKURANGA NDIO KWETU

Assalaam Alyekum waukae,
Kwa niaba yangu binafsi, kwa niaba ya wana jumuiya ya Mkuranga NDIO Kwetu na kwa niaba ya wana Mkuranga wote napenda kuwa taarifu rasmi kikao cha Kesho tarehe 03/03/2012 baina ya Bodi ya shule ya Mwinyi Sekondari, Uongozi wa shule na wawakilishi wa wana jumuiya ya Mkuranga NDIO Kwetu. Lengo la kikao hicho ni kujadili changamoto za Elimu ( Kushuka Kiwango cha Ufaulu) na kujaribu kutafuta suluhisho ya changamoto hizo.

Pia tutajaribu kujadili uzoefu mdogo uliopatikana katika hamasa ya ya ELIMU zilizofanyika Mwinyi, Kiparang'anda na Lukanga Sekondari.

Mkuranga NDIO Kwetu itawakilishwa na
  1. Baraka Mwago
  2. Farida Mgomi
  3. Ramadhani Magimba
  4. Zawady Ally
  5. Rashid Selungwi 
  6. Hidaya Omari 
  7. Nyimgeni Mohamed 
Wote wenye ajenda yeyote inayodhaniwa ni muhimu jadiliwa ziwakilishwe kwa wa wakilishi wetu/wenu

Wasalaam,
Baraka Mwago
M/Kiti Mkuranga NDIO Kwetu