TUIJENGE MKURANGA YA KESHO, WAKATI NI HUU
Ndg
zangu tuna kazi kubwa ya kutimiza ndoto, njozi na hamasa yetu kutimia.
Miezi michache imebaki kwa Ndg zetu kidato cha nne kuanza mitihani ya
taifa na programu yetu ya kufundisha inasusua kwa kukosa fedha za
kuerejesha nauli kwa wanaojitolea kufundisha na kuwapa hamasa ndogo.
HALI IKOJE?
Mkoa wa Pwani ni wa pili toka mwisho baada ya Shinyanga kwa viwango
vibovu vya ufaulu na Mkuranga ni ya mwisho kimkoa. Mkuranga Ndio Kwetu,
hatuwezi ikimbia aibu hii, hatuwezi kuwa na fahari ya kwetu ikiwa
tunazalisha sifuri kwa wingi kimkoa na kitaifa
NINI CHA KUFANYA?
Ili tujipambanue tuko tofauti na wengine na tudhibitishe kweli tuna
nia, uchungu na mapenzi ya dhati na Mkuranga basi tutimize wajibu wetu
na ahadi zetu.
KIVIPI
1. Wale tulio mbali na Mkuranga na
tunao uwezo wa kuchangia kile kima angalau 20,000/= kwa mwezi tufanye
hivyo. Allah atufanyie wepesi Inshallah kwa kutoa na wenye uwezi zaidi
tuchangie zaidi, Kwa niaba yenu nimemshukuru kaka yetu Abdallah Ulega amehaidi kuchangia Million moja mwisho wa mwezi huu
2. Wale waliomaliza kidato cha sita, vyuo pamoja na wale walioko vyuoni
na hata makazini kama una likizo na nafasi inapatikana tujitoe kidhati
kwa sasa katika kipindi hiki cha lala salama kulikoni kusubir aibu
itufike tena na tuanze kumtafuta mchawi wetu.
3. Wenye kuweza
kupata nyenzo na vifaa vya kufundishia, kujifunzia au kwa namna yeyote
inaweza rahisisha zoezi hili wakati ndio huu
MICHANGO INAKUSANYWA NA NANI?
Bado michango inakusanywa na dada/mama/shangazi yetu Mh Farida Mgomi,
kwa niaba yenu nilimshukuru pia kwa kuendelea kukubali jukumu hili hata
baada ya kupewa majukumu makubwa ya kitaifa. Tunaweza tuma kwa M-Pesa
na Tigo Pesa kwa no zake 0715 371919 au 0757 371919.
NANI ANARATIBU ZOEZI LA KUFUNDISHA?
Kwa wale Allah atawapatia wakati wa kujitolea kudundisha mnaweza wasiliana na katibu wa sekretariat yetu Nyimgeni Mohamedi
ndio anaratibu zoezi hili zima. Shukrani kwake na timu nzima
inayoendela kupambana kwa niaba yetu japo kwa mazingira magumu na
tunawaacha wapweke kana kwamba ni programu yao pekee.
Tuwasiliane kwa maswali zaidi,
Baraka Mwago,
Kaimu M/kiti wa jumuiya hii,
0713/787 094 824
barakamwago@yahoo.com
www.mkurangandiokwetu.blogspot.com