KARIBU MKURANGA

Tuesday, July 17, 2012

 TUIJENGE MKURANGA YA KESHO, WAKATI NI HUU

Ndg zangu tuna kazi kubwa ya kutimiza ndoto, njozi na hamasa yetu kutimia. Miezi michache imebaki kwa Ndg zetu kidato cha nne kuanza mitihani ya taifa na programu yetu ya kufundisha inasusua kwa kukosa fedha za kuerejesha nauli kwa wanaojitolea kufundisha na kuwapa hamasa ndogo.

HALI IKOJE?
Mkoa wa Pwani ni wa pili toka mwisho baada ya Shinyanga kwa viwango vibovu vya ufaulu na Mkuranga ni ya mwisho kimkoa. Mkuranga Ndio Kwetu, hatuwezi ikimbia aibu hii, hatuwezi kuwa na fahari ya kwetu ikiwa tunazalisha sifuri kwa wingi kimkoa na kitaifa

NINI CHA KUFANYA?
Ili tujipambanue tuko tofauti na wengine na tudhibitishe kweli tuna nia, uchungu na mapenzi ya dhati na Mkuranga basi tutimize wajibu wetu na ahadi zetu.

KIVIPI
1. Wale tulio mbali na Mkuranga na tunao uwezo wa kuchangia kile kima angalau 20,000/= kwa mwezi tufanye hivyo. Allah atufanyie wepesi Inshallah kwa kutoa na wenye uwezi zaidi tuchangie zaidi, Kwa niaba yenu nimemshukuru kaka yetu Abdallah Ulega amehaidi kuchangia Million moja mwisho wa mwezi huu

2. Wale waliomaliza kidato cha sita, vyuo pamoja na wale walioko vyuoni na hata makazini kama una likizo na nafasi inapatikana tujitoe kidhati kwa sasa katika kipindi hiki cha lala salama kulikoni kusubir aibu itufike tena na tuanze kumtafuta mchawi wetu.

3. Wenye kuweza kupata nyenzo na vifaa vya kufundishia, kujifunzia au kwa namna yeyote inaweza rahisisha zoezi hili wakati ndio huu

MICHANGO INAKUSANYWA NA NANI?
Bado michango inakusanywa na dada/mama/shangazi yetu Mh Farida Mgomi, kwa niaba yenu nilimshukuru pia kwa kuendelea kukubali jukumu hili hata baada ya kupewa majukumu makubwa ya kitaifa. Tunaweza tuma kwa M-Pesa na Tigo Pesa kwa no zake 0715 371919 au 0757 371919.

NANI ANARATIBU ZOEZI LA KUFUNDISHA?
Kwa wale Allah atawapatia wakati wa kujitolea kudundisha mnaweza wasiliana na katibu wa sekretariat yetu Nyimgeni Mohamedi ndio anaratibu zoezi hili zima. Shukrani kwake na timu nzima inayoendela kupambana kwa niaba yetu japo kwa mazingira magumu na tunawaacha wapweke kana kwamba ni programu yao pekee.

Tuwasiliane kwa maswali zaidi,

Baraka Mwago,
Kaimu M/kiti wa jumuiya hii,
0713/787 094 824
barakamwago@yahoo.com
www.mkurangandiokwetu.blogspot.com


No comments:

Post a Comment