KARIBU MKURANGA

Sunday, June 10, 2012

KENYA YAPATA MSIBA WA WAZIRI WA USALAMA WA NDANI

           Marehemu Prof. George Saitoti enzi za uhai wake
 
Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.

Miili ya marehemu imeungua vibaya na moto hivyo utambuzi wa miili hiyo utakuwa mgumu.Mkuu wa polisi aelekea eneo la tukio.Chanzo cha ajali hiyo mbaya bado hakijajulikana.Tetesi zimeshaanza kuhusisha ajali hii na kikundi cha ugaidi cha Al Shabab cha nchini Somalia pamoja na mbio za urais nchini Kenya.RI.P marehemu wote.
You might also like:


No comments:

Post a Comment