KARIBU MKURANGA

Tuesday, June 5, 2012

FARIDA MGOMI NA ABDALLAH ULEGA KAWENI MABALOZI WAZURI WA WANA MKURANGA


Hakika ilikuwa ni faraja na habari njema kusikia vijana wazawa na wapigania harakati za maendeleo ya Wilaya ya Mkuranga ndg Abdallah Ulega na ndg Farida Mgomi kupata uteuzi wa Ukuu wa Wilaya. Farida Mgomi awa mkuu wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara na Abdallah Ulega awa mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Uteuzi wao si heshima na faraja kwao pekee yao bali ni heshima na faraja kubwa kwa wana Mkuranga wote, wakubwa, watoto na Vijana. Imani kubwa aliyokuwa nayo Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete kwao ni Heshima Kubwa kwa jamii nzima ya wana mkuranga na imefuta dhana kuwa Mkuranga na Pwani hakuna watu.

Rai ya wana Mkuranga kwa ndugu zetu ambao ni wana jumuiya ya Mkuranga Ndio Kwetu watawakilisha vyema taswira na jina la Mkuranga na kwamwe uteuzi huo hautawafanya waache kupigania harakati za Maendeleo ya  Mkuranga, uteuzi wao utafungua fursa nyingine zaidi kwa vijana na jamii ya Mkuranga kwa ujumla.

MKURANGA ITAJENGWA NA WANA MKURANGA WENYE MAPENZI NA NIA YA DHATI NA MKURANGA YENYEWE

No comments:

Post a Comment